Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyang Suleiman Masoud Nchambi (CCM) leo Ijumaa Mei 8,2020 amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga na akikabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu uchumi.
Hata hivyo Mshtakiwa Suleiman Nchambi hakutakiwa kujibu mashtaka hayo kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na imeahirishwa hadi siku ya Jumatatu wiki ijayo ambapo Mbunge huyo amepelekwa mahabusu.
Social Plugin