Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amewaonya maafisa Tarafa mkoani humo, kutogeuza pikipiki za Serikali kwa matumizi ya bodaboda, bali zitumike kuhudumia wananchi.
Telack alibainisha hayo jana wakati akikabidhi pikipiki kwa maafisa Tarafa 14 wa mkoani Shinyanga, zilizotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi.
Alisema pikipiki hizo zimetolewa kwa ajili ya kuhudumia wananchi, hivyo hatarajii kusikia zimegeuzwa kwa matumizi ya boda boda.
"Mheshimiwa Rais wetu ametoa pikipiki hizi kwa maafisa tarafa, ili kuwaboreshea utendaji wenu wa kazi, na kuwahudumia wananchi ipasavyo kwa kutatua kero zao, hivyo sitatarajia kusikia zimegeuka kuwa boda boda," alisema Telack.
"Pia naagiza mjiepushe na masuala ya Rushwa kwenye utendaji wenu wa kazi, bali mchape kazi kwa weledi, pamoja na kutunza Ofisi mpya ambazo tumewajengea ili zidumu kwa muda mrefu," aliongeza.
Naye Afisa tarafa ya Old Shinyanga Neema Mkandala, akizungumza kwa niaba ya wenzake, alitoa shukrani kwa Rais John Magufuli kwa pikipiki hizo huku, wakiahidi kwenda kuchapa kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza mara baada ya kumaliza kuwakabidhi pikipiki maafisa tarafa 14 mkoani humo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kulia, akimkabidhi pikipiki afisa tarafa ya Old Shinyanga Neema Mkandala kwa niaba ya wenzake 14.
Afisa tarafa ya Old Shinyanga Neema Mkandala, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake.
Maafisa tarafa wakijaribishia pikipiki mara baada ya kumaliza kukabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Maafisa tarafa wakiwa kwenye pikipiki walizokabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, zilizotolewa na Rais John Magufuli.
Pikipiki walizokabidhiwa maafisa tarafa mkoani Shinyanga.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Social Plugin