Mahakama ya Mombasa
Taarifa kutoka Mahakama ya Mombasa nchini Kenya, zinaripoti kuwa jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Maurice Ochieng, ameachiwa kwa dhamana baada ya kumshambulia jirani yake na kumng'oa jino.
Maurice Ochieng amefanya kisa hicho, baada ya jirani yake huyo ambaye ni muuza maji aitwaye Harrison Charo, kumtumia ujumbe wa kimahaba binti yake.
Kisa hicho kimetokea siku ya Jumapili Mei 10, 2020 na inasemekana Maurice Ochieng, alikutana na kumshambulia Harrison Charo kwenye shughuli zake za biashara ya maji huku akitaka kujua kwanini alimtumia meseji za mapenzi mtoto wake.
Hata hivyo mtuhumiwa Ochieng alikana madai hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya Tsh Milioni 2 na kesi hiyo itasikilizwa tena siku ya Ijumaa Mei 15,2020.
Chanzo Tuko News, Kenya
Social Plugin