Spika mpya wa Bunge la Iran Mohammad Ghalibaf amesema leo majadaliano yoyote na Marekani hayatokuwa na manufaa na badala yake mkakati wa Iran unapaswa kuwa wa kulipa kisasi na siyo mazungumzo.
Ghalibaf, kamanda wa zamani wa kikosi cha anga katika jeshi la walinzi wa mapinduzi ametoa matamshi hayo alipokuwa akitoa hotuba ya kwanza mbele ya bunge la Iran .
Spika huyo aliyechaguliwa hivi karibuni amesema ni lazima Iran ilenge kuondoa uwepo wa majeshi ya Marekani kwenye kanda hiyo na kulipa kisasi kwa kifo cha kamanda wa ngazi ya juu wa jeshi la Iran Qassim Soleimani aliyeuliwa na Marekani mnamo mwezi Januari.
Kadhalika Ghalibaf ametoa wito kwa serikali kuimarisha mahusiano na mataifa mengine yenye nguvu yaliyo rafiki na Iran ambayo mara zote yamewaunga mkono katika kipindi kigumu.
Social Plugin