Spika wa Bunge ,Job Ndugai amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kujiandaa kulipa gharama za kesi iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho,Tundu Lissu.
Spika Ndugai amesema amepewa nakala ya hukumu kutoka Mahakama Kuu iliyotupilia mbali rufaa yake namba 42 ya mwaka 2019 iliyowashitaki yeye (Spika ) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu ubunge wa Singida Mashariki.
“Nimepata nakala ya hukumu Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali walikuwa wameshitakiwa na bwana Tundu Lissu katika shauri la Mahakama Kuu namba 42 la mwaka 2019 ya kwamba Mahakama imetupilia mbali madai hayo tena kwa gharama kwa hio wajiandae kulipa ” amesema Spika Ndugai
Lissu alifungua kesi hiyo akipinga kuvuliwa ubunge wake wa Singida Mashariki ambalo kwa sasa linaongozwa na Miraji Mtaturu kutoka Chama cha Mapinduzi.
Social Plugin