Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 6, 2020 amewataka wabunge wa Chadema waliosusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona kurudi haraka bungeni.
Spika ndugai amesema endapo watakaidi agizo hilo la kurudi bungeni basi itawalazimu siku watakayo rudi wawe na cheti kinachoonesha kuwa wamepima ugonjwa wa Corona na majibu yake na kurudisha pesa walizolipwa ambazo ni posho za vikao la sivyo hatua zaidi zitachukuliwa.
"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1 - 17 Jumla ya zaidi Sh Mil 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh Mil 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Mil 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.
Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa; "Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na tangazo hilo kwa sababu Mbowe hana mamlaka ya kuitisha utoro wa wiki mbili kwa Wabunge, anajaribu kuwa kama Prefect wa Shule ya Sekondari, japo wameambiana kubaki Dodoma lakini wanazurura nchi nzima, wabunge hao popote walipo warudi bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao".
Social Plugin