Mahakama Kuu nchini Marekani imeaiagiza Sudani kuwalipa fidia waathiriwa wa shambulio la mwaka 1998 katika balozi za Marekani Nairobi nchini Kenya na Dar es salaam nchini Tanzania.
Uamuzi huo wa Mahakama Kuu nchini Marekani unawahusisha raia wa Marekani, wafanyakazi wa balozi hizo na wakandarasi.
Uamuzi huo unajiri wakati ambapo serikali ya Sudani inapigania kuondolewa katika orodha ya Marekani ya mataifa yanayofadhili ugaidi.
Uamuzi huo ulioungwa mkono na majaji wengi unamaanisha kwamba takriban Dola Milioni 800m kati ya Dola bilioni 4 ambazo ziliamrishwa na mahakama hiyo kuwafidia mwaka 2011 zimerejeshwa.
Mwaka 2017 , Sudan ilifanikiwa kuupinga uamuzi huo ikihoji kwamba walipatiwa fidia hiyo chini ya marekebisho ya sheria ya 2008 ambayo haiwezi kusimamia kitu kilichotokea miaka 20 iliopita.
Shambulio hilo la al-Qaeda kwenye balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania liligharimu maisha ya watu 224. Tangu mwaka 2001, karibu watu 600 wameendelea kuomba Sudan iwalipe fidia kwa sababu wakati huo Khartoum iliwapa hifadhi wanamgambo wa Kiislamu pamoja na Osama bin Laden.
Kesi hiyo ilifikishwa hadi Mahakama Kuu ambayo ilithibitisha kwamba Khartoum inapaswa kulipa fidia.
Social Plugin