Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), leo tar. 14 Mei, 2020 ametembelea shehena ya awali ya tani 600 iliyopokelewa katika bandari ya Mwanza.
Mhe. Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa Sukari iliyoingia nchini na kusambazwa Mikoa mbalimbali ya Nchi inaenda kumaliza changamoto ya upatikanaji wa Sukari.
Amewaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha sukari inauzwa kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali huku akiahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara watakaopandisha bei.
Social Plugin