Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia
akimkabidhi vifaa vya 85 vitakavyotumika kwa ajili ya usafi kwenye
wilaya tatu zilizopo mkoani Tanga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
kushoto ili viweze kusambazwa maeneo mbalimbali
ikiwemo masokoni,hospitalini na stendi sambamba na kujenga masinki ya
kunawia
mikono kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Upendo Lugongo na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally halfa ya makabidhiano hayo
ilifanyika mjini Pangani msaada huo ulitolewa na Tanga Uwasa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia
akimkabidhi vifaa vya 85 vitakavyotumika kwa ajili ya usafi kwenye
wilaya tatu zilizopo mkoani Tanga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
kushoto ili
viweze kusambazwa maeneo mbalimbali
ikiwemo masokoni,hospitalini na stendi sambamba na kujenga masinki ya
kunawia
mikono kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Meneja
wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Upendo Lugongo na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally halfa hiyo ilifanyika mjini Pangani msaada huo ulitolewa na Tanga Uwasa
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo leo
kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akinawa mikono na vifaa hivyo
ambavyo vimetolewa na Tanga Uwasa kwa wilaya tatu mkoani Tanga wakati
wa halfa ya makabidhiano leo kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi
Geofrey Hilly
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga (Tanga Uwasa) wametoa vifaa 85 kwa wilaya tatu zilizopo mkoani
Tanga ili viweze kusambazwa maeneo mbalimbali ikiwemo
masokoni,hospitalini na stendi sambamba na kujenga masinki ya kunawia
mikono.
Vifaa hivyo vitagawiwa kwenye wilaya tatu ambazo ni
wilaya ya Pangani, Muheza na Tanga ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha
wanakabiliana na usafi wa kudumu kwenye maeneo mbalimbali
Akizungumza
wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine
Shigella, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba vifaa
hivyo ni ndoo kumi kwa kila wilaya ambazo zitakuwa zimewekwa na koki kwa
ajili ya kunawia vilivyotolewa na mamlaka hiyo.
“Kwa Pangani
tumeleta ndoo 10 na Muheza ndoo 10 ambazo zitasambazwa kwenye maeneo
yaliyolengwa pia tutaendelea kujenga masinki ya kunawia kwa ajili ya
usafi na sio Corona pekee yake “Alisema
Awali akizungumza wakati
akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema kwa
niaba ya ya Serikali ya Mkoa aliishukuru Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira (Tanga Uwasa) kwa kutoa msaada huo wa vifaa ambavyo
vitatumika kwenye usafi wa kunawa mikono.
Alisema jambo hilo ni
muhimu sana la kupambana na magonjwa mbalimbali na kwamba haulengi
kwenye Corona kwa sababu tayari wamekwisha malizana nao huku akieleza
kwamba msaada huo umefika wakati muafaka katika kuhakikisha jamii
inanawa mikono na kujiweka kwenye hali ya usafi kila wakati.
“Msaada
huu aulengi Corona kwa sababu tumekwisha malizana nalo una lenga
kukabiliana na tatizo lolote hivyo nikuombe Mwenyekiti wa Halmashauri
vifaa hivyo viwekwe kwenye maeneo yaliyokusudiwa na visiende kukwekwa
kwenye stoo”Alisema RC Shigella.
“Lakini pia vifaa hivyo viwekwe
kwenye maeneo ambayo watu wanaenda kunawa mikono kama sehemu ya
utamaduni kila wakati na tuhakikishe tunanawa mikono kila wakati na huu
uwe kama ustaarabu wetu”Alisema
Naye kwa upande wake Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally alisema kwamba wanaishukuruTanga
Uwasa kwa msaada huo baada ya Mbunge wao Jumaa Aweso kupeleka ombi nao
wakaona wamsaidie msaada huo ambao utawasaidia kupelekwa maeneo
mbalimbali ili kusaidia usafi.
“Tanga uwasa walipewa ombi kuhusu
suala hilo nao wakaona waweze kuja kutukabidhi leo lakini kubwa tuna
mshukuru mbunge wetu Jumaa Aweso kwa kuwa mbunifu na kuweza kututafutia
ndoo hizo “Alisema
Social Plugin