Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TBS YATAJA MAMBO 7 YA KUZINGATIA KWA WAZALISHAJI NA WATUMIAJI WA BARAKOA ZA VITAMBAA KATIKA MAPAMBANO YA CORONA


Katika kuendelea kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona nchini, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa katika uzalishaji na utumiaji wa barakoa za kitambaa (cloth face mask).


Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile inaeleza matakwa ya msingi ambayo yanapaswa kuzingatiwa na wazalishaji, wasambazaji na watumiaji wa barakoa hizo.

Matakwa hayo ni;
  1.     Kitambaa kiwe cha pamba (cotton) kwa asilimia 100
  2.     Kitambaa kiwe na uzito wa GSM 90-130
  3.     Barakoa iwe na tabaka (layers) zisizopungua mbili
  4.     Barakoa iwe na uwezo wa kuruhusu upumuaji kwa      urahisi
  5.     Iweze kuvalia na kufunika pua na mdomo vizuri
  6.     Kitambaa kisiwe chenye kuchuja rangi (kwa kitambaa chenye rangi)
  7.     Iweze kufuliwa na kunyooshwa kwa pasi au kuanikwa juani bila kuathiri ubora wa kitambaa
Aidha, shirika hilo limesema linaendelea na maandalizi ya viwango mbalimbali vya vifaa vya kinga binafsi (Personal Protective Equipments-PPE).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com