Mlipuko wa homa ya kirusi cha corona umeleta athari nyingi kwa jamii zetu na kuathiri kwa kiasi kikubwa wananchi na watoa huduma ya afya barani Afrika na duniani kote.
Nchi mbalimbali zimechukua hatua kusaidia taasisi za afya kama hospitali kuweza kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa ambayo kwa wakati mmoja inahitaji wahudumu wa afya, dawa na vifaa.
Njia mojawapo kusaidia hilo ni kupunguza uwezekano wa maambukizi na tumeona hatua kama kufunga shule, mahoteli na kukataza mikusanyiko. Serikali ya Tanzania pia imetangaza kujenga hospitali mpya kubwa ya magonjwa ya milipuko jijini Dar es Salaam.
Huku serikali ikichukua hatua hizo, kampuni za kiteknolojia nazo zimeongeza nguvu kusaidia watoa huduma za afya kuweza kufanya kazi yao vyema katika ongezeko hili la wagonjwa si wa corona peke yake lakini hata wa maradhi mengine.
Teknolojia imeweza kupunguza msongamano katika maeneo ya kutoa huduma za afya kwa namna nyingi. Kwanza imewezesha mawasiliano, ambayo mtu anaweza kupiga simu na kueleza anavyojisikia na kupata ushauri moja kwa moja kupitia simu badala ya kufika hospitali.
Pili imesaidia kwa upatikanaji wa mtandao wa intaneti ambayo ni chanzo cha watu kuweza kupata taarifa mbalimbali za afya kupitia mtandao.
Tatu, zipo kampuni za teknolojia na mawasiliano ambazo zimeenda mbali zaidi hadi kuwapa wateja wake uwezo wa kupata bima ya afya, ajali na ya maisha. Tigo ni moja ya kampuni nchini Tanzania ambayo imefanya hivyo.
Huduma ya Tigo ya Bima Mkononi inawapa wateja wake uwezo wa kujiunga na bima kupitia simu zao na kupata faida ya sapoti ya kifedha kwa kila siku ambayo mteja au mnufaika wa familia anapokuwa amelazwa hospitali.
Tigo pia imeshirikiana na Wizara ya Afya na kutengeneza mfumo wa usajili wa vizazi jambo linalosaidia upatikanaji wa haraka wa vyeti vya kuzaliwa na utunzaji mzuri wa taarifa za vizazi nchini.
Hatua na ubunifu wa namna hii katika mawasiliano na teknolojia katika huduma ya afya ni muhimu ili kuwezesha wananchi kupata huduma kwa haraka na ubora pale wanapozihitaji.
Mbali na changamoto tunazopitia katika janga hili la corona, tusisahau namna ambavyo ubunifu na teknolojia vinaweza kutusaidia kubaki salama.
Social Plugin