Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TRUMP ASAINI SHERIA INAYOLENGA KUIBANA MITANDAO YA KIJAMII IKIWEMO TWITTER, FACEBOOK NA YOUTUBE


Rais Donald Trump wa Marekani jana Alhamisi alisaini Amri ya Utendaji (Executive Order on Preventing Online Censorship) inayolenga kuongeza uwezo wa serikali kusimamia  na kuibana mitandao ya kijamii.

Amri hiyo inalenga kampuni zilizopewa ulinzi wa kisheria kupitia kifungu cha 230 cha Sheria ya mawasiliano ya staha (Communications Decency Act). 

Kwa mujibu wa kifungu hicho, kampuni kubwa za mitandao ya kijamii hazitashitakiwa kutokana na maudhui yaliyowekwa na watumiaji kwenye tovuti zao lakini zinaweza kuhusika kwa upande wa usamaria mwema wa kuondoa maudhui hayo mtandaoni ambayo labda yana maudhui ya unyanyasaji, chuki na yanaaibisha

Amri hiyo imekuja siku mbili baada ya mtandao wa kijamii wa Twitter, kwa mara ya kwanza, kuweka alama ya onyo kwenye jumbe mbili alizoandika rais Trump kwenye ukurasa wake, inayowashauri wasomaji "kuhakiki ukweli wa taarifa hizo".


Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Trump, baada ya rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta huwa una udanganyifu mwingi.

Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema "Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo, na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com