TRUMP ATUMIA VETO KUUKATAA MUSWADA WA KONGRESI ULIOMPUNGUZIA MAMLAKA YA KUANZISHA VITA DHIDI YA IRAN


Rais Donald Trump wa Marekani ametumia mamlaka yake ya veto kuukataa muswada uliopitishwa na Kongresi, ambao umetaka mamlaka aliyopewa ya kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Iran yapunguzwe.

Kufuatia hatua hiyo ya Trump, muswada huo sasa unahitaji theluthi mbili za kura za uungaji mkono za bunge hilo la Marekani ili uweze kuwa sheria moja kwa moja bila kuhitaji kusainiwa na rais wa nchi hiyo.

Tarehe 14 ya mwezi uliopita wa Aprili, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi alisaini azimio la kupunguza mamlaka ya rais wa nchi hiyo ya kuanzisha vita dhidi ya Iran ambalo lilipitishwa na baraza hilo mwezi Machi.

Vitisho vya kuanzisha vita dhidi ya Iran ambavyo Rais wa Marekani Donald Trump alivitoa baada ya mauaji ya Kamanda wa Jeshi la Iran,  Qassem Soleimani na watu alioandamana nao yaliyofanywa na jeshi  la Marekani, vilizidi kulitia wasiwasi bunge la nchi hiyo na kuwafanya wabunge wa chama cha Democrat wachukue hatua ili kupunguza mamlaka ya Trump yanayohusiana na kuanzisha vita dhidi ya Iran.

-Parstoday


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post