Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwa ndani ya gari la Wagonjwa ‘Ambulance’ iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi amekabidhi gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ufadhili wa Global Fund - RSSH kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mhe. Kwandikwa amekabidhi gari hilo leo Jumamosi Mei 9,2020 katika hafla fupi ya makabidhiano ambayo imehudhuriwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Ushetu pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Mhe. Kwandikwa amesema gari hilo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya afya ili wananchi waweze kupata huduma bora za afya.
“Naishukuru serikali kwa kusikia kilio cha wana Ushetu kuhusu changamoto ya gari la wagonjwa lakini pia nimshukuru pacha wangu Mhe. Azza kwa ushirikiano anaoendelea kuutoa katika jimbo hili na leo tumefanikiwa kupata gari kwa ajili ya wananchi”,alisema Mhe. Kwandikwa.
“Gari hili linaweza pia kutumika kuhudumia pia maeneo yanayozunguka kituo cha Mbika kama vile Ulowa na Uyogo ingawa kituo chake kikubwa kitakuwa ni hapa Mbika.Naomba gari hili litunzwe na litumike kwa malengo yaliyokusudiwa”,alisema Kwandikwa.
Katika hatua nyingine Mhe. Kwandikwa amekabidhi ndoo 28 za kunawia mikono zitakazogawiwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Ushetu, vitakasa mikono ‘ Sanitizers’,sabuni za maji, Barakoa ’Surgical Masks’ kwa ajili ya watumishi wa afya kituo cha afya Mbika.
Mhe. Kwandikwa pia amechangia shilingi Milioni 1 kwa ajili ya SACCOS ya akina Mama Uyogo huku Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad akichangia shilingi 300,000/= kwa ajili ya SACCOS hiyo.
Awali akizungumza, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad aliishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi ya kuleta gari kwa ajili ya wagonjwa aliloliomba kwa ajili ya Kituo cha Afya Mbika akieleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
“Mwaka 2018 Wakati Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifanya ziara katika Jimbo la Ushetu nilimuomba atusaidie kupata gari la wagonjwa,alikubali na leo hii gari limefika katika kituo cha afya cha Mbika ili wananchi wapate huduma. Namshukuru sana kaka yangu Elias Kwandikwa kwa ushirikiano anaotoa kwa wabunge wa mkoa wa Shinyanga katika kuwahudumia wananchi”,alisema Mhe. Azza.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha aliwapongeza wabunge hao (Azza Hilal na Elias Kwandikwa) kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha kusaidia wananchi huku akibainisha kuwa wabunge hao wamekuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo.
“Mhe. Kwandikwa na Azza ni wabunge ambao wapo mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo,wao badala ya kujifungia wao wanatoka kuja kwa wananchi. Wabunge hawa siyo mara yao ya kwanza kushirikiana na wananchi kutekeleza ilani ya uchaguzi",alisema Macha.
“Tunaamini hata kama ni kesho yake tarehe 25 ni siku ya kupiga kura wao wakileta msaada tarehe 24 nikiwaona siku hiyo nitaona ni mwendelezo wala mimi siwezi kuona ni maajabu lakini tukipata watu wanakuja siku za mwisho mwisho hatukuwahi kuwaona tutauliza nyie mlikuwa wapi.
Niseme kwa hakika mnachofanya ni mwendelezo wa yale mmekuwa mkifanya msije mkaacha kuleta mlivyobakiza mkasema mkija watasema mnafanya kampeni,tunaendelea pale tulipoachia…Wanaoanza ndiyo tutakuwa na mashaka nao”,alisema Macha.
“Kwa kweli naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru sana na tunawaona nyinyi Mhe. Azza na Mhe. Kwandikwa ni askari mlio mstari wa mbele na tunaendelea kuwakaribisha na nyinyi kwetu siyo wageni,mmezoea kuja kila siku. Na wale wengine ambao wanajaribu jaribu kupiga jalamba au kutaka kupiga jalamba waangalie umbali kutoka hawa walipo na walivyovifanya. Tuwape nafasi watekeleze majukumu kwa jinsi ambavyo sisi tunaona ni watu wanaotusaidia”,aliongeza Mkuu huyo wa wilaya.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ufadhili wa Global Fund - RSSH kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu leo Jumamosi Mei 9,2020. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiishukuru serikali kwa kuleta gari la Wagonjwa ‘Ambulance’ kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad aliishukuru serikali kwa kutekeleza ahadi ya kuleta gari kwa ajili ya wagonjwa aliloliomba kwa ajili ya Kituo cha Afya Mbika akieleza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiishukuru serikali kuleta gari la wagonjwa Ushetu na kuwapongeza wabunge hao (Azza Hilal na Elias Kwandikwa) kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiuonesha kusaidia wananchi huku akibainisha kuwa wabunge hao wamekuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli za maendeleo.
Gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi (katikati) akikata utepe wakati akiwakabidhi viongozi wa halmashauri ya Ushetu gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwasha gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwa ndani ya gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akiwa akiwasha king'ora ndani ya gari la Wagonjwa ‘Ambulance’lililotolewa na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kituo cha afya cha Mbika kata ya Ushetu halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa akiwa ameshikilia sehemu ya Sanitizers na sabuni, barakoa alizotoa kwa ajili ya watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Mbika na vituo vingine vya afya katika Jimbo la Ushetu ili kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa akimkabidhi Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Mhe. Michael Matomora Sanitizers kwa ajili ya watoa huduma za afya katika kituo cha afya cha Mbika na vituo vingine vya afya kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa akimkabidhi Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu, Mhe. Michael Matomora ndoo moja kati ya ndoo 28 alizotoa kwa ajili ya kuwekwa katika maeneo mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu wananchi wanawe mikono kwa maji na sabuni ili kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Ndoo 28 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa kwa ajili ya kuwekwa katika maeneo mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu wananchi wanawe mikono kwa maji na sabuni ili kujikinga na maambukizi ya COVID - 19.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Elias Kwandikwa akikabidhi shilingi Milioni 1 kwa ajili ya SACCOS ya akina Mama Uyogo ambapo pia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga, Mhe, Azza Hilal Hamad akichangia shilingi 300,000/= kwa ajili ya SACCOS hiyo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog