Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali yake itawekeza kwa makampuni yote makubwa yanayofanya jitihada za kutafuta chanjo ya virusi vya corona na kwamba imepunguza idadi ya makampuni hayo hadi kufikia 14, huku akitoa ahadi ya kuyapunguza zaidi.
Katika mkutano wake uliofanyikia Ikulu ya Marekani, ambapo ulihudhuriwa na maafisa wengi wa Ikulu hiyo wakiwa wamevaa barakoa, lakini yeye akiwa hajavaa, Trump alionesha matumaini kwamba kinga ya maradhi ya COVID-19 itapatikana kabla ya kumalizika mwaka huu.
Na kuongeza kusema serikali yake itashiriki vyema katika usambazaji wa chanjo hiyo pale tu, itakapopatikana.
Hayo yanajiri wakati takwimu mpya zilizotolewa na chuo kikuu cha John Hopkins zinaonesha vifo vipya 1,680 ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliopita na kufanya idadi ya vifo kufika 88,507.
Maambukizi nchini Marekani yamefika 1,484,287 na waliopona ni 327,751
Social Plugin