Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona nchini Kenya imeongezeka hadi 700 baada ya wagonjwa wapya 28 kuthibitishwa katika kipindi cha saa 24.
Katibu mtendaji katika wizara ya Afya Rashid Aman amesema kwamba kati ya wagonjwa hao wapya 10 wanatoka Momabasa , 9 kutoka kajiado na 7 kutoka Nairobi huku 2 wakitoka Wajir.
Wagonjwa wote tisa kutoka Kajiado ni Wakenya ambao ni madereva wa malori ya masafa marefu ambao walipimwa katika mpaka wa Namanga.
Jumla ya sampuli 841 zilifanyiwa vipimo katika kipindi cha saa 24 zilizopita
Afisa huyo wa afya ametangaza wagonjwa wengine 12 waliopona na hivyobasi kufanya idadi ya wale waliopona kufikia 251.
Social Plugin