Taarifa ya Wizara ya afya nchini uganda kwa vyombo vya habari inaashiria maambukizi mapya 13 ya kirusi cha Corona na kuifikisha idadi ya visa kuwa 139.
Wagonjwa wapya wote ni Madereva wa Malori ambapo kati yao Waganda ni 7, Wakenya 5 na Raia wa Eritrea mmoja aliyepitia Sudan Kusini,Kenya,Tanzania na kisha Uganda kupitia mpaka wa Mtukula.
Takribani sampuli 2,104 zimefanyiwa vipimo,miongoni mwazo 1741 zikiwa za madereva huku 363 kutoka maeneo tofauti ya ndani mwa Uganda.
🔸All 363 community samples have tested negative for COVID-19.🔹Total samples tested today at @UVRIug are 2,104— Ministry of Health- Uganda (@MinofHealthUG) May 13, 2020
Social Plugin