Wizara ya Afya nchini Uganda imesema Madereva wanne wa malori wamethibitishwa kuwa na Virusi vya Corona na kufanya idadi ya visa nchini humo kufikia 126.
Wawili kati ya Wagonjwa wapya ni Waganda huku wengine wakiwa ni raia wa Kenya na Tanzania. Waganda na Mkenya wanaaminika kuingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu na Mtanzania alipimwa katika mpaka wa Mutukula
Wamegundulika baada ya sampuli 1,478 za madereva wa malori kupimwa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi Uganda. Hadi sasa sampuli zaidi ya 10,000 za madereva wa malori zimepimwa
🔸All 233 community samples have tested negative for COVID-19.🔹 Total samples tested today: 1711#STAYSAFEUG— Ministry of Health- Uganda (@MinofHealthUG) May 12, 2020
Social Plugin