Waziri wa Katiba na sheria Mhe.Mwigulu Nchemba amesema kitendo cha baadhi ya Wabunge wa Upinzani kususia vikao vya Bunge kwa kuogopa Corona ni ishara ya kutengeneza madaraja na mpango wa kushusha uchumi wa nchi.
Waziri Nchemba amesema hayo jana Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya wizara ya Viwanda na Biashara ya makadirio na matumizi kwa mwaka wa fedha,2020/2021 ambapo amewataka Watanzania kuacha kusikiliza miluzi ambayo inapotosha taifa.
Waziri Nchemba amesema Maisha ya Watanzania mara nyingi hayana akiba hivyo kitendo cha watanzania kujifungia ndani bila kufanya kazi kwa tahadhari ya Corona kama wanavyoshauri baadhi ya wabunge wa Upinzani panaweza kutengeneza majanga mengine hivyo wanatakiwa kufuata ushauri uliotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli wa kuchapa kazi na kuondoa hofu juu ya Corona na kubainisha kuwa janga halikimbiwi.
Waziri Nchemba ameteuliwa na Rais Dokt John Pombe Magufuli hivi karibuni kuiongoza Wizara ya Katiba na Sheria tukio lililofanyika Mjini Chato mkoani Geita baada ya aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo Dkt.Balozi Augustine Mahiga kufariki Dunia
Social Plugin