Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WENYE VIRUSI VYA CORONA NCHINI KENYA WAFIKA 490


Kenya imethibitisha maambukizi mapya 25 ya virusi vya Corona na kufikisha 490 waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo kufikia sasa.

Wizara ya afya inasema kuwa visa 15 vinatoka jijini Nairobi na 10 kutoka kaunti ya Mombasa.

Wote wakiwa ni wakenya ambao hawana historia ya kusafiri nje ya nchi.

Naibu waziri wa afya Dkt Mercy Mwangangi anasema kuwa sampuli 1012 zilifanyiwa vipimo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Aidha watu 6 zaidi wamepona na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kufikisha 173 waliopona kufikia sasa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com