Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kumalizika kwa mlipuko wa Virusi vya Corona bado ni safari ndefu kufuatia ongezeko la maambukizi duniani.
Kauli yake inakuja baada ya Idadi kubwa zaidi kurekodiwa kwa siku moja tangu kuanza kwa mlipuko wa Corona, amabpo visa 106,000 vimeripotiwa katika Shirika hilo ndani ya saa 24 zilizopita.
Dkt. Tedros ameweka wazi wasiwasi uliopo kuhusu ongezeko la maambukizi kwenye nchi masikini na zenye uchumi wa kati. Aidha, Wataalamu wameonya kuwa idadi halisi ya maambukizi inaweza kuwa kubwa zaidi.
Hadi kufika sasa takribani Visa 5,129,453 vya wagonjwa wa covid -19 vimerekodiwa ulimwenguni, Wagonjwa 2,044,614 wamepona na 331,021 wamepoteza maisha.
Social Plugin