Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro
Na mwandishi wetu,Shinyanga Press Club Blog
Watu nane wamepoteza maisha katika ajali ya gari na wengine watano kujeruhiwa baada ya Lori mali ya Texas Hardware kugonga Tela la trekta kwa nyuma na kukosa mwelekeo kisha kuligonga gari la abiria 'Hiace' na kusababisha vifo.
Ajali hiyo ilitokea jana Juni 10 majira ya saa 9:45 usiku katika barabara ya Mwanza -Musoma eneo la Ihayabuyaga Kata ya Bukandwe wilayani Magu mkoani Mwanza ambapo tayari wanamshikilia dereva wa lori Boniphace Cliphord Tuju(37) mkazi wa mwanza-Nera
Taarifa iliyotolewa leo Juni 11 na kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro imesema kuwa, dereva huyo alikuwa anaendesha gari lenye namba za usajili T.322 DCB na Trailer T.1351 DCA na lilikuwa likitoka wilaya ya Busega kwenda Mwanza.
Kamanda Muliro amesema Lori hilo liligonga tela ya trakta kwa nyuma ambayo ilikuwa haina taa za nyuma yenye namba za usajili T.952 DGW, baada ya kuligonga ilihama njia na kugongana na gari iliyokuwa na abiria kutoka mwanza kwenda magu yenye namba za usajili T.775 DEG.
Alisema gari ya abiria aina ya Nissan inayomilikiwa na george philipo@msangi ambaye alikuwa dereva wa gari hiyo ambaye alifariki kwenye ajali na abiria wake waliopoteza maisha wote wakiwa ni wanaume na watano kujeruhiwa.
Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na miili yao kutambuliwa ni George Msangi dereva wa Hiace mkazi wa Magu,Hamis Masige(35) mwalimu wa Luhenge secondary mkazi wa Lugeye na waliofariki wengine 6 bado hawajatambulika wote ni wanaume.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao wanapatiwa matibabu hospitali ya Bugando kuwa ni Ayubu Mindule Mratibu elimu Kata ya Chabula mkazi wa nyanguge,Elias Lutandula(46)mkulima mkazi wa Nyanguge.
Wengine ni Kasabuku Kishela(32)msukuma mkazi wa Magu, Edibini Makubo (20) mwanafunzi wa kidato cha sita Bariadi high school mkazi wa Nyanguge na Elias Francis(44)mkazi wa nyanguge ambaye amelazwa hospitali ya Magu.
Social Plugin