Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis ametangaza kuwaunga mkono wananchi wa Marekani wanaondamana kulaani ubaguzi wa rangi na mienendo ya polisi ya Marekani hususan dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika.
Mattis alitangaza msimamo huo katika taarifa iliyochapishwa jana Jumatano na gazeti la The Atlantic, ambapo amemtuhumu Trump kuwa anajaribu kuwagawanya Wamarekani kimatabaka.
Ameeleza bayana kuwa, "Donald Trump ni rais wa kwanza katika uhai wangu ambaye hawaunganishi Wamarekani, bali hata hajifanyi kana kwamba anajaribu kuwaunganisha."
Amesema taifa hili linashuhudia matokeo ya jitihada za makusudi za miaka mitatu za Trump za kuwagawa wananchi wa Marekani.
James Mattis amesema ;, "tunaweza kuungana bila yeye (Trump), hili si jambo jepesi, lakini linawezekana kwa ushirikiano."
Kadhalika amekosoa hatua ya rais huyo kutumia jeshi la taifa kuzima maandamano ya kiraia, ambayo ni haki ya msingi iliyoanishwa kwenye katiba ya nchi hiyo.
Mattis ambaye ni jenerali mstaafu aliachia ngazi mwishoni mwa mwezi Februari mwaka 2018, baada ya kuhitalifiana na Trump
Kama jibu lake kuhusu ukosoaji huo, Trump alituma mfululizo wa ujumbe kwenye Twitter ambapo alisema..."Sikupenda mtindo wake( James Mattis ) wa uongozi au yeye mwenyewe sikumpenda na wengine wengi wanakubaliana na hilo, "Afadhali aliondoka mapema"
...His primary strength was not military, but rather personal public relations. I gave him a new life, things to do, and battles to win, but he seldom “brought home the bacon”. I didn’t like his “leadership” style or much else about him, and many others agree. Glad he is gone!— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) June 4, 2020
Wananchi wa Marekani wamekuwa wakiandamana kwa zaidi ya wiki moja sasa, tangu alipouawa kikatili na polisi mweupe, George Floyd, Mmarekani mweusi katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesota.