Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge limefanya azimio La Kumpongeza Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kwa Namna Alivyoliongoza Taifa Katika Mapambano Dhidi Ya Janga La UgonjwaWa Corona (Covid-19).
Akiwasilisha azimio hilo jana Juni 9,2020 Bungeni jijini Dodoma mbunge wa VITI MAALUM Esther Mmasi amesema katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona Rais alitumia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo kukataa kuiga mtindo wa kufunga mipaka na kuwafungia wananchi wake wasitoke nje tofauti na viongozi wa Mataifa mengine waliofunga mipaka ya nchi zao na kuzuia watu wao kutokanje (lockdown) .
Hivyo Mhe.Mmasi amesema kwa kuzingatia hali hiyo, Rais Magufuli aliruhusu shughuli za kiuchumi na baadhi ya shughuli za kijamii ziendelee kwa tahadhari na kuwahimiza wananchi kuzingatia maelekezo na miongozo ya wataalam.
Wakichangia Michango yao kuhusu mjadala wa azimio hilo la kumpongeza Rais,baadhi ya Wabunge akiwemo Mbunge wa Rombo Mashariki Joseph Selasini amesema Rais Magufuli amesaidia kuondoa hofu kwa Watanzania ,mbunge wa Viti Maalum Christina Ishengoma akitoa pongezi kwa kuruhusu ibaada huku Mbunge wa Viti Maalum Nagma Giga akisema Rais Magufuli amekuwa Mzalendo wa Kweli kwa Taifa la Tanzania. ==>>Lisome Tamko Zima Hapo Chini
Social Plugin