Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais John Magufuli, leo amechukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama chake kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Rais Magufuli amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally kwenye Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dodoma.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Rais Magufuli amesema anaanza mapema mchakato wa kutafuta wadhamini ili awahi kurejesha fomu hiyo mapema.
Mwenyekiti huyo wa CCM amesema amekuwa akipigiwa simu na makada wa chama hicho, ambao wamemuahidi kumdhamini.
“Naomba nianze zoezi hili la kutafuta wadhamini, nitaenda mikoa yote kwa sababu nimekuwa nikipigiwa simu wakisema wanataka kunidhamini hivyo nitarejesha fomu yangu kwa wakati,” amesema Rais Magufuli.
Social Plugin