Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Lucas Mgonja,
akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu wakati wa ujazaji fomu za
kumdhamini mgombea urais wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori akizungumza na wajumbe wa
Halmashauri Kuu ya wilaya hiyo wakati wa kumdhamini mgombea urais wa
CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo, Chifu Sylevester Yared (kushoto), akiwa
na Katibu wa UWT wa wilaya hiyo, Janeth Mnyaga (kulia) wakiongoza
wajumbe katika ujazaji fomu za kumdhamini mgombea urais wa CCM, Rais Dk.
John Magufuli
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ubungo, wakiwa wakisubiri kujaza
fomu za kumdhamini mgombea urais wa CCM, Rais Dk. John Magufuli
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja ameongoza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, kujaza fomu za kumdhamini mgombea urais wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Rais Magufuli amechukua fomu ya kuwania tena urais kwa kipindi cha pili jana jijini Dodoma na ameanza kusaka wadhamini 250 mikoani kama utaratibu wa CCM unavyoelekeza.
Taarifa ilitolewa leo na Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi, ilieleza kuwa wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ubungo , wameshiriki zoezi hilo kwa ngazi ya wilaya.
“Zoezi la udhamini kwa Wilaya yetu ya Ubungo, limehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Lucas Mgonja, Katibu wa CCM Wilaya Chifu Sylevester Yared pamoja na kamisaa wa chama Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori,” imeeleza taarifa hiyo.
Akizungumza na wajumbe hao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja, alisema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwao kwani wanaamini Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maoni na ataendelea kuifanyia mema Tanzania.
“Ubungo tunasema kwa kauli moja kwamba Magufuki anatosha, tunamwamini na tumemkubali na tunahkika atatuvusha tena.
Miaka mitano ya kwanza hakika ametenda kazi kubwa na kila Mtanzani ni shuhuda nasi Ubungo alitupendelea kwa kuwa na miradi mikubwa ikiwamo Ubungo Inter Change pamoja na barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha kwetu ni heshima kubwa.
“Si hili tu hata ukiangalia miradi ya maji, ujenzi wa shule na zahanati pamoja na hospitali za wilaya nasi Ubungo ni sehemu ya wanufaika wakubwa wa miradi hii, kwa hakika Rais Magufuli ameitendea haki CCM na aliahidi na ametekeleza kila sekta kama ilani ya chama ilivyoelekeza,” amesema Mgonja
Social Plugin