Chama cha Upinzani cha CHAUMMA, kimetangaza rasmi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wake, Hashim Rungwe Spunda amesema wanavikaribisha vyama vingine kuungana nao wakati ambao CHAUMMA inaelekekea kuchukua dola.
Rungwe amesema, hivi karibuni Chaumma itatoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu za wanachama wake watakaohitaji kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
Wakati huo huo, Rungwe amesema Chaumma imekamilisha kuandaa ilani yake ya uchaguzi na kwamba kiko katika mchakato wa kuiwasilisha katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Aidha, Rungwe ameomba wananchi wenye mapenzi mema na chama hicho, kuchangia fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za kampeni.
Social Plugin