Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Donald Trump atishia kutuma jeshi kukabiliana na waandamanaji nchini humo

Rais wa Marekani Donald Trump ameahidi kumaliza maandamano ya vurugu ambayo yameikumba miji mikubwa nchini humo tangu kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46.

George Floyd alifariki baada ya maafisa wa polisi wa Minneapolis kumbana kwa kutumia goti shingoni na mgongoni, uchunguzi wa kimatibabu uliosimamiwa na familia ya Floyd umebaini.

Rais wa Marekani pia alitangaza kwamba matukio ambayo yalifanyika Jumapili Mei 31 katika mji mkuu wa nchi hiyo ni "aibu", na kuyachukulia kama vitendo vya "kigaidi ndani ya nchi". Ametoa wito kwa magavana wa majimbo kuchukua maamuzi muhimu "kukabiliana na maandamano".

Wakati huo huo, vikosi vya usalama vimetumia gesi ya machozi kwa waandamanaji waliokusanyika nje ya ikulu ya White House.

Rais wa Marekani ametangaza sheria kuhusu uasi ambayo inamruhusu kutumia jeshi

"Ninavitaka vikosi vya ulizi na usalama kumaliza ghasia na visa vya uporaji vinavyoendelea, na kulinda haki za Wamarekani, "alisema.

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia kukutana kwa faragha na msimamizi wake mkuu wa sheria , kufuatia maandamano ya vurugu yalioshuhudiwa katika miji kadhaa nchini humo, kupinga ubaguzi na ukatili wa polisi katika wakati huu wa janga la Corona.

Trump hajatoa tamko lolote kuzungumzia mzozo huo unaozidi lakini ameandika tweet kadhaa akiwaelezea waandamanaji kama vibaka na kuwahimiza mameya na magava kuchukuwa hatua kali zaidi. Alitishia pia kutumia jeshi lakini mshauri wake wa usalama wa taifa amesema serikali bado haiwezi kutumia udhibiti juu ya vikosi vya ulinzi wa taifa.

Lakini hadi sasa hakuna Gavana aliyetoa wito kwa jeshi kuingilia kati . Wengi wao wamebaini kwamba kutumia jeshi kunaweza sababisha hali inakuwa ngumu zaidi, ameripoti mwandishi wetu wa Washington, Anne Corpet.

-RFI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com