Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FELIX MKOSAMALI AHAMA NCCR- MAGEUZI NA KUTIMKIA CHADEMA


Aliyewahi kuwa Mbunge wa Muhambwe Mkoani Kigoma kupitia Nccr-Mageuzi Felix Mkosamali, amekihama chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na  Chadema nakutangaza nia ya kuwania ubunge wa Jimbo la Muhambwe kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.



“Nimehama chama cha NCCR-Mageuzi kwasababu kimekuwa kama kinyonga hakieleweki kipo CCM au upinzani, ni chama ambacho kimekuwa hakifanyi kazi yoyote ya kisiasa kwa miaka mitano sasa kimeanza kuweka wagombea kwenye majimbo ya Chadema,” amesema na kuongeza.

“Nimeona Chadema ndio chama sahihi kugombea ubunge kwasababu kuna wanasiasa wenye msiamamo wa kisaiasa na wenye kudai katiba mpya”.

Amesema kuwa amekihama chama hicho ili aendelee kupigania mambo ya msingi na si kujipendekeza na kuwa anaamini wanaohama vyama ni haki yao lakini wengi wanaitumia vibaya haki hiyo kwasababu ya njaa na kushibisha matumbo yao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com