Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KAMPUNI YA VINYWAJI VIKALI EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KISASA KUJIKINGA NA CORONA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akinawa mikono kwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga inayotengeneza vinywaji vya Diamond Rock na Hansons Choice imekabidhi msaada wa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona vyenye thamani vya shilingi Milioni 8 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.



Vifaa vilivyotolewa na Kampuni hiyo ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga ni pamoja na kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki chenye thamani ya shilingi Milioni 6.8 kikiwa na masinki matano na tenki la maji lenye ujazo wa lita 1000 na vifaa vingine vya kujikinga na COVID-19 ikiwemo Vitakasa mikono,barakoa,gloves, pamba, sabuni za maji, cord clamp na pulse Oximeter vyenye thamani ya shilingi milioni 1.2.

Msaada huo umekabidhiwa leo Alhamis Juni 4,2020 na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.

Akikabidhi vifaa hivyo, Gasper Kileo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) amesema vifaa hivyo vitatumika katika kuiongezea nguvu serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

“Ninaishukuru sana serikali  ya awamu ya tano inayoongozwa na Amiri Jeshi wetu Mkuu, Rais wetu Mpendwa, Dkt. John Pombe Magufuli namna ilivyopambana na ugonjwa wa COVID – 19. Tumepambana na COVID-19 tofauti na nchi zote duniani na sasa wote ni mashahidi kwenye vyombo mbalimbali vya habari na Mitandao ya Kijamii kwamba dunia sasa inaangalia Tanzania imefanya nini kuiondoa Corona. wenzetu ndiyo wanafuta kile tunachofanya Tanzania”,amesema Kileo.

“Nimpongeze pia Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack kwa namna mnavyopambana dhidi ya Corona. Lakini pia niwapongeze Madaktari wetu wote nchi nzima mmepambana kwa kushirikiana na serikali na Mungu ametusaidia tumeweza. Naomba tuendelee kupambana mpaka pale Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli atakaposema silaha zetu tuziweke chini”,ameongeza Kileo.

Mkurugenzi huyo pia amewashauri wananchi kuendelea kunawa mikono na kwamba zoezi hilo liwe endelevu hata siku watakapotangaziwa kuwa Corona imefutika nchini Tanzania.

Akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ameishukuru Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa mchango huo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya Corona.

“Mheshimiwa MNEC uliniambia utaleta vifaa kwa ajili ya kupambana na Corona lakini sikujua kama utaleta vikubwa namna hii. Umetuwekea masinki ya kunawia mikono na tenki kubwa la maji na umeweka hadi kivuli ili watu wetu wanaponawa mikono wawe kivulini. Mwenyezi Mungu akubariki sana na abariki Biashara yako na shughuli unazofanya ziendelee na kukua ili uweze kutupa misaada mingine zaidi”,amesema Telack.

“Kimsingi mimi nimepokea vifaa hivi kwa niaba ya wananchi lakini hawa wananchi wanaonawa hapa wataendelea kukuombea kwa Mungu. Umetengeneza kitu kikubwa sana na pengine ndiyo maana walikuchagua kuwa MNEC wao hata wale wasiokuwa wa CCM sasa wanaona jinsi viongozi wa CCM na serikali ya CCM inavyojali wananchi. Huu ni mfano wa kutosha,niombe na viongozi wengine waige mfano wako”,amesema Mkuu huyo wa mkoa.

“Umeenda kisasa zaidi,umetuletea vifaa vya kisasa,na naomba uongozi wa hospitali hii uweke mtu wa kuwaelekeza wananchi namna ya kutumia kifaa hiki, wasianze kugusa gusa wakavunja hapa,wajue kwamba akisogeza mikono yake maji yanatoka. Na pengine hapa patakuwa mahali pa kujifunzia masuala ya teknolojia ya kisasa.

Yaani MNEC unafundisha watu teknolojia ambazo zipo,wataambiana ukienda hospitali,ukisogeza tu mkono maji yanatoka,yaani hiyo nayo ni sehemu ya kujifunzia. Ninategemea tutapata wageni wengi zaidi,wengine watakuja kunawa tu mikono ili waone jinsi maji yanavyoka bila kugusa,wananchi watakuja kujifunza. RMO naomba vifaa hivi vitunzwe ili visiharibike”,amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika hatua nyingine,Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kuendelea kunawa mikono mara kwa mara ili kupunguza maradhi mengine yanayotokana na kutozingatia taratibu za afya

“Kunawa mikono ni ustaarabu. Sasa hivi siyo COVID -19 peke yake tumegundua kwamba kunawa mikono kunatupunguzia maradhi mengine kama vile tumbo na kuharisha,huko wodini sasa hivi watu waliokuwa wanakuja kwa matatizo ya tumbo na kuhara wamepungua kwa kiasi kikubwa sana”,amesema.

“Niwaombe wananchi wa Shinyanga hii tabia ya kunawa mikono iwe endelevu siyo kwa sababu ya Corona tu,hata baada ya Corona unaingia hospitali nawa mikono yako,unaingia sokoni nawa mikono yako ili pia tuweze kupunguza maradhi mengine yanayotokana na kutozingatia taratibu za afya”,ameongeza Telack.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Timoth Sosoma ameishukuru Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa msaada huo na kueleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona huku akiwataka wananchi wasiwe wagumu kunawa mikono.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Muonekano wa Masinki ya kunawia mikono bila kugusa koki ambayo ni sehemu ya kifaa cha kisasa cha kunawia mikono kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga inayotengeneza vinywaji vya Diamond Rock na Hansons Choice  kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Juni 4,2020. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (katikati) akikata utepe wakati akipokea kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona kutoka Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (aliyevaa kilemba cha bluu) namna ya kunawa mikono kwa kutumia kifaa cha kisasa cha kunawia mikono.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akinawa mikono kwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akinawa mikono kwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akinawa mikono kwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akinawa mikono kwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiishukuru Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa mchango wa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu palipowekwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono iliyotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu palipowekwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono iliyotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu wa tanki la maji ambalo ni sehemu ya kifaa cha kisasa cha kunawia mikono kilichotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu palipowekwa kifaa cha kisasa cha kunawia mikono iliyotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa kwa ajili ya kujikinga na COVID-19 ikiwemo Vitakasa mikono,barakoa,gloves, pamba,cord clamp na pulse Oximeter vyenye thamani ya shilingi milioni 1.2 vilivyotolewa na Kampuni ya Uzalishaji Vinywaji Vikali ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (aliyevaa kilemba cha bluu kushoto) kifaa cha kisasa cha kunawia mikono bila kugusa koki na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona  katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo akiipongeza serikali inayoongozwa na  Rais Dkt. John Pombe Magufuli namna ilivyopambana na ugonjwa wa COVID – 19. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (wa tatu kulia) akiishukuru Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa mchango wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack sabuni ya kunawia mikono ili kukabiliana na COVID - 19 katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga, Gasper Kileo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack Vitakasa mikono ili kukabiliana na COVID - 19 katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Timoth Sosoma akiishukuru Kampuni ya East African Spirits (T) Limited Shinyanga kwa msaada wa vifaa vya kujikinga na COVID- 19 ambavyo vitasaidia katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona katika hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com