Idara ya polisi mjini Minneapolis katika jimbo la Minnesota nchini Marekani itafanyiwa mabadiliko makubwa kutokana na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd.
Halmashauri ya jiji hilo imekubaliana kuivunja kabisa idara ya polisi na kuweka muundo mpya wa utendaji kazi wa polisi.
Hayo ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Baraza la mji huo Lisa Bender.
Floyd aliuawa mikononi mwa polisi chini ya wiki mbili zilizopita mjini humo tukio ambalo lilizusha maandamano ya kitaifa nchini Marekani na mengine mengi katika nchi mbalimbali.
Mwaka jana, afisa mmoja wa polisi wa zamani mjini Minneapolis alihukumiwa kifungo cha miaka 12 na miezi sita jela kwa kumpiga risasi na kumuuwa mwanamke mweupe wa Australia ambaye hakuwa na silaha yoyote, wakati akitoa habari ya tukio la uhalifu.
-DW
Social Plugin