Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amemhamisha Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana amehamishwa kwenda kuwa Afisa Mnadhimu shule ya Polisi Moshi.
Hayo yameelewza leo Jumatano June 24, 2020 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini SACP David Misime wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.
Aidha, Miseme amesema kuwa IGP Sirro, amemhamisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Bunge, Dodoma ACP Emmanuel Lukula kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na nafasi yake inachukuliwa na ACP Andrew Satta ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Social Plugin