Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JOGOO ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUPIGA KELELE AAGA DUNIA


Jogoo Maurice, ambaye alishtakiwa kwa sababu ya kuwika kila asubuhi, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 6.

Jogoo huyo alishtakiwa kwa kupiga kelele na wanandoa waliostaafu ambao walikuwa wakati wakiwa likizoni nchini Ufaransa kisiwa cha Oléron.

Mmiliki wa jogoo hilo, Corinne Fesseau, alisema kile alichokuwa anafanya jogoo wake ni kuwika tu kawaida kama jogoo wengine.

Maurice pamoja na waliomshtaki, hakuna aliyekuwepo mahakamani ana kwa ana wakati kesi hiyo inasikilizwa.

Lakini ogoo maurice alipata umaarufu wa kimataifa na kuwa nembo ya kampeni ya kulinda sauti kote nchini Ufaransa - baada kujipata katika mgogoro wa kisheria juu ya kupiga kelele.

Aliyeshtaki alilalamika kwamba Bi. Fesseau, mmiliki wa jogoo, alianzisha kubisha baada ya kupewa taarifa na kusababisha mgogoro.

Bi. Fesseau, na wafuasi wake kwenye jamii hiyo, walisema kwamba jogoo ni sehemu ya maisha ya watu wa vijijini na haina maana kusema kwamba jogoo huyo anyamazishwe.

Now ikiwa kuna kile ambacho kingehitajika kufanywa kwa Maurice basi mahakama ilihitajika kuingilia kati na kutoa uamuzi wake Septemba.Corinne Fesseau akiwa na jogoo wake

Mwaka 2019, uamuzi wa mahakama ulimpendelea jogoo Maurice na kuishi katika siku zake zote zilizokuwa zimesalia katika kisiwa cha Oléron.

Jogoo huyo alikufa Mei lakini mmiliki wake akasubiri muda mwafaka wa kutangaza kifo chake.

"Nilijiambia kwamba kwasababu ya hatua za kutotoka nje, watu tayari wana mengi ya kukabiliana nayo," Corinne Fesseau alinukuliwa akisema hivyo katika kituo kimoja cha redio cha Ufaransa.

"Tumenunua jogoo mpya na huyo pia tumemuita Maurice - pia nae anawika kama yule wa kwanza tu. Lakini hawezi kuwa Maurice wetu."
Bi. Fesseau alijaribu kumnyamazisha Maurice - ikiwemo kumfunika kwa shuka

Matatizo ya Maurice yalianza pale wanandoa waliostaafu waliokuwa likizo katika nyumba moja ya kuko huko Oléron walipomshtaki kwa kuwasumbua wakati anawika.

Baada ya hapo jogoo huyo alikuwa maarufu nchini Ufaransa kiasi cha kuwa miongoni mwa nembo za kitaifa na malefu ya watu walitia saini ombi la kutaka kumnusuru.

Walalmishi, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, walijenga nyumba yao ya kupumzika ambayo ni kama eneo lao la kitalii wakati walikizo katika kijiji cha Saint-Pierre-d'Oléron karibia miaka 15iliyopita.

Walisema kwamba moja ya sabab iliyochangia wao kujenga nyumba hiyo kwenye kijiji hicho, ni utulivu wa eneo. Lakinimambo yalianza kubadilika pale jogoo Maurice alipoanza kuwika kila mara tena kwa sauti ya juu mno 2017.Maurice hatanyamazishwa baada ya mahakama kumuunga mkono

Septemba mwaka jana, jaji alitoa umauzi unaompendelea jogoo maurice na kuagiza aliyeshtaki kulipa pauni 1,000 sawa na (£900; $1,100) kama fidia.

"Ushindi huu ni kila mmoja aliyekatika hali kama hii. Ni matumaini yangu mimi nitaweza kutumika kama mfano," Bi Fesseau amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema hivyo wakati huo.
Chanzo - BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com