Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa Bajaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Nyangoma James Mama mwenye Ulemavu wa miguu msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kununulia Bajaji ili imsaidie kuendesha Maisha yake. Pia Rais Dkt. Magufuli aliendesha Mchango kwa Wananchi wengine ambapo waliahidi kumchangia mama huyo kiasi cha Shilingi Milioni 3.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama mwenye Ulemavu wa miguu Nyangoma James mara baada ya kumchangia kiasi cha Shilingi Milioni 5. kushoto aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makore.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa hamasa pamoja na Wananchi wa Ubungo mara baada ya kuwahutubia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika eneo la Ubungo Darajani mara baada ya kuzungumza na Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Ubungo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili wakati akitokea Mkoani Dodoma.
PICHA NA IKULU
Social Plugin