Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi amesema kuwa Rais Magufuli anapaswa kuingizwa kwenye vitabu vya Guinness, vitabu ambavyo vimesheheni maajabu na historia ambazo zimevunja rekodi kwa Dunia nzima.
Katambi ameyabainisha hayo hivi karibuni wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kueleza kuwa anatamani Rais Magufuli awekwe huko kwa sababu ni Rais anayesikika duniani kwa utendaji wake wa kazi, pamoja na maono makubwa aliyokuwa nayo.
"Ni Rais mwenye maono na upendo na ni Rais ambaye amefanya performance ambayo haijawahi kufikiwa kwenye rekodi za Dunia, ni kwa vile tu nchi za ughaibuni hawapendi kuonekana wao wako nyuma na hawapendi kuona watu weusi wamefanya vitu 'Extra Ordinary', Rais huyu alipaswa kuingia kwenye vitabu vya Guinness" amesema Katambi.
Haya yote yanajiri baada ya Rais Magufuli kumkumbusha suala la kuoa, kwa kuwa Jiji la Dodoma haliwezi kuongozwa na watu ambao hawajaoa.
Chanzo - EATV
Social Plugin