Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) leo Ijumaa Juni 5, 2020 kimeitembelea Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC) katika ofisi zake zilizopo mtaa wa Miti Mirefu mjini Shinyanga kwa lengo la kujenga Mahusiano mema, kutangaza mipango mikakati ya chama hicho itakayotekelezwa ndani ya miaka mitatu.
Kiongozi wa msafara wa mawakili hao, Magdalena Mlolere ambaye ni mwakilishi kutoka TLS makao makuu Dar es Salaam amesema kwa sasa wamejipanga kuja na mpango mkakati wa miaka mitatu kuisadia jamii katika suala la sheria.
Ameyataja baadhi ya mambo yatakayokuwa kwenye mkakati huo kuwa ni pamoja na kufanya kazi na serikali za mitaa kwa kushauri juu ya uandaaji wa sheria ndogo na kanuni, pia kushirikiana na asasi za kiraia kuzifahamu sheria za uanzishwaji na uendeshaji wake.
Kwa upande wake Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), Estomine Henry amesema milango ipo wazi kwa chama hicho kufanya kazi na waandishi wa mkoa huo, kuwasaidia katika masuala ya kisheria na kushirikiana katika utekelezaji wa mikakati yao waliyoitangaza.
Naye Mwenyekiti Msaidizi wa TLS Kanda ya Shinyanga, Vicent Masalu amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na mipango ya kutafuta ofisi za uhakika ndani ya mkoa huo ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kutekeleza shughuli zao kwa ukaribu zaidi.
Msafara huo uliambatana na mawakili Magdalena Mlolere mwakilishi kutoka TLS makao makuu Dar es Salaam, Martin Masanja ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili TLS mkoa wa Shinyanga, Vicent Masalu, Lucy Mwang’ombe na Mary Mwanjela ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya msaada wa kisheria mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya mawakili kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wakijadili jambo walipotembelea ofisi ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) mjini Shinyanga.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakifuatilia mazungumzo wakati Chama cha Mawakili Tanganyika walipoitembelea ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga.
Mwakilishi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kutoka makao makuu Dar es Salaam, Magdalena Mlolere akizungumza wakati alipotembelea Klabu ya waandishi wa habari mkoani shinyanga.
Baadhi ya mawakili kutoka TLS, Martin Masanja na Mary Mwanjela wakisikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga wakati wa kikao cha uhusiano mwema kilichofanyika leo Juni 5, 2020 katika ofisi za SPC mjini Shinyanga.
Mmoja wa Waandishi wa habari, Kareny Masasy akizungumza katika kikao hicho.
Mawakili Martin Masanja na Mary Mwanjela wakifuatilia mazungumzo.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na mawakili kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) nje ya ofisi ya Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC) mjini Shinyanga.