Jamaa mmoja mwenye miaka 42, kutoka mjini Kakamega nchini Kenya ameaga dunia asubuhi ya Jumatano, Juni 24, 2020 baada ya kudaiwa kutumia dawa za kupandisha ashiki za kimapenzi/ kuongeza nguvu za kiume 'Viagra' kupita kiasi.
OCPD wa Kakamega ya kati, David Kabena, alisema mwathiriwa aliyetambuliwa kama Munala, alikodisha chumba kimoja cha lojing'i mjini humo pamoja na mwanamke mmoja mwenye miaka 31, aliyetambuliwa kama Anyango, kutoka Kaunti ya Siaya Jumanne, Juni 23,2020 mchana.
Kwa mujibu wa ripoti ya K24, wawili hao waliagiza chajio 'chakula' kabla ya kuelekea chumbani katika hoteli ya Amazon huku jamaa huyo akikosa kula chochote.
“Wawili hao waliagiza chakula kabla ya kuelekea chumbani katika Hoteli ya Amazon.Na ni mrembo huyo pekee ambaye alikuwa, amekula" ,alielezea Kabena.
Mapema Jumatano asubuhi, Anyango alijitoma kutoka chumbani humo na kumuambia meneja wa hoteli hiyo kuwa mpenzi wake aliaga dunia baada ya kutumia dawa za kupandisha ashiki za kimapenzi(viagra) kupita kiasi.
Mkuu wa hoteli hiyo aliwaita maafisa wa polisi, ambao waliwasili na kuupeleka mwili wake katika makafani ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kaunti ya Kakamega ambapo ulifanyiwa upasuaji Jumatano mchana.
Matokeo ya upasuaji yalionyesha kuwa marehemu aliaga dunia kutokana na mshtuko wa moyo ambayo inaaminika kusababishwa na dawa hizo.
Mwendazake alikuwa ameoa na kujaliwa mtoto wa kiume mwenye miaka minane pamoja na mke wake ambaye wameishi pamoja kwa miaka kumi.
Mjane wa jamaa huyo alisema hajafanya mapenzi na mume wake kwa mwaka mmoja sasa. OCPD alisema bado uchunguzi unaendelea kuhusu kifo cha mwanamume huyo.
CHANZO - TUKO SWAHILI
Social Plugin