Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KAHAMA YAKAGUA UJENZI WA MRADI WA MAJI NGOGWA - KITWANA....DC MACHA ATAKA 'WANAOJIWEKA LOCKDOWN WAJE SITE'


Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kahama ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha imetembelea na kukagua ujenzi wa Mradi wa Maji Safi Ngogwa – Kitwana katika halmashauri ya Mji Kahama ambao unatarajiwa kukamilika Mwezi Agosti mwaka huu ukigharimu jumla ya shilingi Bilioni 2.4

Mradi huo unasimamiwa na kutekelezwa  na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA) pamoja na Wakala wa Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga  na wilaya ya Kahama.

Akizungumza leo Ijumaa Juni 5,2020 katika eneo la mradi huo unaotekelezwa katika kata za Ngogwa na Busoka,Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha ameipongeza SHUWASA,KUWASA na RUWASA namna wanavyotekeleza mradi huo kwa kasi kubwa.

“Nawapongeza sana SHUWASA,KUWASA na RUWASA kwa umoja wenu na  ushirikiano na wananchi mnaoendelea nao katika kuhakikisha ujenzi wa mradi unakamilika kabla ya Mwezi Agosti mwaka huu. Lengo la serikali ni kuona wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama”,alisema Macha ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama.

Aidha Macha alisema utekelezaji wa mradi wa Majisafi Ngogwa – Kitwana ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo kwani wananchi wanahitaji kuona maendeleo badala ya maneno tu.

“Tunatekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Wapuuzeni watu wanaokaa Hotelini na kuzungumzia masuala ya Ilani ya CCM. Huwezi kuelewa mambo mazuri yanayofanywa na serikali ukiwa Mjini umejiweka Karantini ‘Lockdown’, Wanaosema Ilani ya CCM haitekelezwi waje huku  ‘site’ wajionee wenyewe jinsi miradi inavyotelezwa”,alisema Macha.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kukubali mabomba ya maji yapite kwenye maeneo yao kwani mradi huo hauna fungu la fidia ya ardhi na mali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi alisema chanzo cha maji ya  Mradi wa Kitwana – Ngogwa ni kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama – Shinyanga (KASHWASA).

“Eneo lililopendekezwa na wataalamu kama chanzo cha maji katika mradi wa Kitwana – Ngogwa ni Nyamhela ambapo limepita bomba la chuma lenye kipenyo cha mm.750 linalopeleka maji katika tenki linalomilikiwa na KUWASA na kuhudumia mji wa Kahama”,alisema Kifizi.

Alisema mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wapatao 27,095 baada ya kukamilika na wakazi wapatao 44,618 mwaka 2033 kwa kuwa mradi umesanifiwa kutoka huduma kwa kipindi cha miaka 15 na unatekelezwa na kutumia wataalamu wa ndani ‘ Force Account’.

Kifizi alieleza lengo kuu la mradi huo ni kufikisha huduma ya majisafi katika kata za Ngogwa na Busoka ambapo tayari ujenzi wa tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’ lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa umefikia asilimia 95.

Alisema pia ujenzi wa tenki la juu kwenye mwinuko ‘Riser’ la mita 12 lenye ukubwa wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana umefikia asilimia 45 na hatua inayofuata sasa ni uchimbaji wa mtaro mkuu  na ulazaji wa bomba kuu kilomita 15.26.



Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kahama imejionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi tenki la kukusanyia maji la ardhini katika kijiji cha Ngogwa, tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ katika kijiji cha Kitwana na eneo la chanzo cha maji katika mradi wa Kitwana – Ngogwa Nyamhela katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiongoza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama kuelekea katika Mradi wa Maji Safi Ngogwa – Kitwana katika halmashauri ya Mji Kahama unaotekelezwa na SHUWASA,KUWASA na RUWASA. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha (wa pili kushoto) kuhusu ujenzi wa Mradi wa Maji Safi Ngogwa – Kitwana katika halmashauri ya Mji Kahama ambao unatarajiwa kukamilika Mwezi Agosti mwaka huu ukigharimu jumla ya shilingi Bilioni 2.4
Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama kuhusu ujenzi wa tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa ambao umefikia asilimia 95.
Muonekano ujenzi wa tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa ambao umefikia asilimia 95.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha  akipanda katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa. 
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama  wakipanda katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa. 
Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Ngogwa - Kitwana, Mhandisi Yusuph Katopola kutoka SHUWASA akielezea kuhusu ujenzi wa tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa huku akielezea kuwa ujenzi wa tenki hilo umefikia asilimia 95 na Mradi huo wa maji unatarajiwa kukamilika kabla ya Agosti 31,2020.  
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akiwapongeza SHUWASA,KUWASA na RUWASA kwa kwa kasi wanayoendelea nayo kutekeleza mradi wa Ngogwa - Kitwana akibainisha kuwa utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo kwani wananchi wanahitaji kuona maendeleo badala ya maneno tu.
Mkazi wa Kijiji cha Ngogwa, Sylivester Sita akiishukuru serikali kwa kutekeleza mradi wa maji safi wa Ngogwa - Kitwana ili kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata maji umbali mrefu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha  akishuka katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama,Mhe. Anderson Msumba akishuka (mbele) katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa. Wengine ni maafisa wa SHUWASA,KUWASA na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha, Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Bi. Flaviana Kifizi na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama wakiondoka katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha, Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Bi. Flaviana Kifizi (wa pili kushoto),Meneja wa RUWASA, Kahama Mhandisi Moses Mwampunga na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama wakiondoka katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha, Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Bi. Flaviana Kifizi (wa pili kushoto),Meneja wa RUWASA, Kahama Mhandisi Moses Mwampunga na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama wakiondoka katika tenki la kukusanyia maji la ardhini ‘Ground water tank’  lenye ukubwa wa lita 680,000 katika kijiji cha Ngogwa kata ya Ngogwa.
Hapa ni katika Kijiji cha Kitwana: Pichani ni Muonekano hatua ya ujenzi wa tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ukubwa wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana ambao umefikia asilimia 45.
Kulia ni Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Magige Marwa akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa kwanza kulia) kuhusu ujenzi wa tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ukubwa wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana ambao umefikia asilimia 45. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akipanda katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ukubwa wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 45.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (katikati) akiwa juu ya tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 45. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa polisi wilaya ya Kahama, Lutusyo Mwakyusa. Wa pili kulia ni Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA),Luchanganya Paul.
Muonekano sehemu ya juu ujenzi wa  tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiangalia namna ujenzi wa  tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana unavyoendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akishuka katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama wakishuka katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama wakishuka katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana. wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Bi. Flaviana Kifizi,kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Maji wa Ngogwa - Kitwana, Mhandisi Yusuph Katopola kutoka SHUWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama,maafisa kutoka KUWASA,SHUWASA NA RUWASA wakiwa katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama,maafisa kutoka KUWASA,SHUWASA NA RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama,maafisa kutoka KUWASA,SHUWASA NA RUWASA wakipiga picha ya kumbukumbu katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana.
Hapa ni eneo la Nyamhela ambapo kuna mabomba ya maji. Nyamhela ndiyo chanzo cha maji katika mradi wa Kitwana – Ngogwa ni  ambapo limepita bomba la chuma lenye kipenyo cha mm.750 linalopeleka maji katika tenki la juu kwenye mwinuko ‘riser’ wa mita 12 lenye ujazo wa lita 135,000 katika kijiji cha Kitwana kata ya Kitwana linalomilikiwa na KUWASA na kuhudumia mji wa Kahama.
Mhandisi wa Mipango na Ujenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Magige Marwa na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Luchanganya Paul wakikagua mabomba ya maji katika eneo la Nyamhela.
Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama (KUWASA), Luchanganya Paul akiwaelezea Wajumbe wa Kamatiya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama namna mabomba hayo ya maji yalivyotengenezewa nchini Tanzania yakiwa na uwezo mkubwa wa kuhimili Mgandamizo wa maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiangalia mabomba ya maji katika eneo  la Nyamhela. Nyamhela ndiyo chanzo cha maji katika mradi wa Kitwana – Ngogwa ni  ambapo limepita bomba la chuma lenye kipenyo cha mm.750 
Meneja waWakala wa Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Kahama Mhandisi Moses Mwampunga akielezea namna wanavyoshirikiana na SHUWASA na KUWASA kutekeleza mradi wa maji wa Ngogwa - Kitwana.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama,Mhe. Underson Msumba akielezea namna Halmashauri ya wilaya ya Mji Kahama na wananchi wanavyoshirikiana na SHUWASA,KUWASA na RUWASA kutekeleza mradi wa majisafi Ngogwa -Kitwana ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha  akiwapongeza SHUWASA,RUWASA, KUWASA,Halmashauri ya Mji Kahama na wananchi jinsi wanavyoshirikiana kutekeleza mradi wa Majisafi Ngogwa - Kitwana.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com