MAREKANI NA IRAN WABADILISHANA WAFUNGWA


Iran na Marekani wamebadilishana wafungwa kwa mara nyingine licha ya mvutano mkubwa kati ya nchi hizo mbili hasimu, ishara kwamba mataifa hayo mawili yanaweza kufikia maelewano ya kudumu.

Michael White, askari wa zamani wa kikosi cha wanamaji cha Marekani aliyekamatwa mwezi Julai 2018 nchini Iran, atakuwa "hivi karibuni na familia yake Marekani," Donald Trump amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter, ambaye amesema amezungumza na mateka huyo wa zamani , ambaye kwa sasa yuko nchini Uswisi, na "hivi karibuni atakuwa njiani kulekrea nchini Marekani".

"Asante Iran, hii inaonyesha kuwa mkataba unawezekana!", ameongeza rais wa Marekani, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi, huku akiahidi kuendelea kujikita na "kuachiliwa huru kwa raia wote wa Marekani wanaoshikiliwa Mateka katika nchi za kigeni"- jambo ambalo limeendelea kukaribishwa na Wamarekani wengi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Baada ya tangazo kuhusu Bw. White, Tehran imesema kwamba mwanasayansi wa Iran, Majid Tahéri, aliyekuwa anazuiliwa nchini Marekani "kwa madai yasiyoeleweka", ameachiliwa na serikali ya Washington.

Majid Tahéri alikanusha mashtaka dhidi yake kuhusu ubadhirifu wa kifedha mwezi Desemba, na pia alishtakiwa kwa kutuma zana ya kiufundi nchini Irani kwa kukiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran, lakini jaji wa Marekani aliagiza kuachiliwa kwake huru Alhamisi wiki hii

-RFI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post