Picha haihusiani na habari hapa chini
Na mwandishi wetu- Shinyanga Press Club blog
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la James Mhoja(36)ameuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuua mtoto wa dada yake mtoto Emmanuel John(4) kwa kumkata mapanga wakati akicheza na watoto wenzake nyumbani kwao.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Joseph Paul amesema tukio hilo lilitokea jana Juni 9 majira ya saa 9 alasiri kwenye Mtaa wa Ndala Manispaa ya Shinyanga, wakati mtoto huyo alipokuwa anacheza nje ya nyumba yao ndipo mtu huyo alimvamia na kumshika kisha kuanza kumkata mapanga.
"Mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto huyo naye aliuawa na wananchi kwa kumponda mawe na katika uchunguzi wetu wa awali,tumebaini alikuwa anatatizo la ugonjwa wa akili na bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hili"amesema kaimu Kamanda Paul.
Social Plugin