Picha : BONANZA LA MICHEZO LA MAVETERANI KANDA YA ZIWA LAUNGURUMA UWANJA MPYA WA 'FRESHO COMPLEX' SHINYANGA


Maveterani kutoka Mikoa ya Mwanza (Mwanza Starehe Veterani), Tabora (Unyanyembe Veterani) na Shinyanga (Ammo Veterani /Jeshi Veterani na Shinyanga Veterani) wamekutana katika Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited kwa ajili ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuhamasisha wananchi wafanye mazoezi ili kujenga afya zao pamoja na kushuhudia uwanja mpya wa Fresho Complex.

Bonanza hilo limefanyika leo Jumamosi Juni 6,2020 katika Uwanja Mpya wa Kisasa uliopewa jina la ‘Fresho Complex’ unaojengwa na Mwekezaji Mzawa, Kampuni ya Fresho Investment Company Ltd katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali Justas Kitta.

Akifungua Bonanza hilo katika uwanja huo ulioanza kutumika leo, Kanali Kitta ambaye ni miongoni mwa Wachezaji wa Timu ya Jeshi Veterani alimpongeza Fredy Shoo kuwekeza katika sekta ya Michezo kwa kujenga uwanja wa Mpira wa miguu 

“Mimi nikiwa Mwanamichezo,Mkuu wa taasisi ya serikali, nikupongeze sana ndugu yangu Fresho kwa kazi kubwa uliyoifanya. Hii umejenga ni hospitali, itatibu magonjwa mengi badala ya mtu kwenda hospitali kupata dawa atapata hapa. Magonjwa nyemelezi tutayaondoa kwenye kiwanja hiki”,amesema Kanali Kitta.

“Michezo ni afya na michezo inaleta ushirikiano ndiyo maana tumefika hapa kama watu tunaothamini michezo. Ukifanya michezo ni tiba ya magonjwa mengi hasa ukizingatia kuwa sasa tupo katika Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona kama Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alivyosema kuwa Michezo ni tiba mbadala katika magonjwa mbalimbali na hata hili gonjwa la Corona”,ameeleza Kanali Kitta.

“Tukipata watu watatu wanne kwa Shinyanga hii nafikiri Kimichezo tutapiga hatua kubwa sana.Kwa hiyo nikutie moyo ndugu yangu endelea,na ningependa katika mkoa wetu tuwe na mabonanza kama haya kila mwezi tuhamasishe watu wapende michezo ili kuondokana na magonjwa mbalimbali kwani michezo ni afya”,ameongeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo amesema lengo la kufanya Bonanza hilo la michezo ni kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kutaka Watanzania wawe na afya nzuri na kuweza kupiga vita ugonjwa wa Corona ambapo watu wanaofanya mazoezi wana uwezakano mkubwa wa kushambuliwa na Virusi vya Corona.

Aidha Shoo amesema lengo la kujenga uwanja wa michezo wa ‘Fresho Complex’ ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli katika kufanya watu wakiwemo ,wafanyakazi wa viwandani na serikalini wawe na afya nzuri kwa kufanya mazoezi.

“Tumeanza kujenga uwanja huu mwaka 2017 baada ya ziara ya Rais Magufuli mkoani Shinyanga, tulihamasika kuwa, pamoja na kwamba tunaendelea kujenga viwanda vingine,tumeona tujenge kiwanda cha afya ili kuunga mkono serikali. Pamoja na kwamba ninawekeza katika viwanda nimeona pia niwekeze katika uwanja wa michezo”,amesema Shoo.

“Kingine kilichonisukuma pia kuwekeza katika ujenzi wa uwanja ni kutokana na kwamba mimi ni mchezaji wa Veterani. Wengi wakisikia Veterani wanadhani ni wale wachezaji ambao walikuwa wanacheza katika timu kubwa wakawa wamestaafu. Mimi sikuwahi kucheza Klabu yeyote ya mashindano ya Ligi lakini najiita Veterani kwa sababu ni mchezaji ninayecheza mwenye umri mkubwa”,ameongeza Shoo.

“Niliona tukiwa na uwanja huu Watu wenye umri mkubwa katika eneo hili tutakuwa tunafanya mazoezi katika uwanja huu. Na kutokana na agizo la Mheshimiwa Rais kuwa wananchi wafanye mazoezi siku za Jumamosi,hivyo siku za Jumamosi uwanja huu tutautoa bure ili wananchi wafanye mazoezi hapa”,amesema.

Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kwamba uwanja huo utakuwa wa kibiashara lakini siku za Jumamosi atatoa bure kwa siku ambazo serikali imesema ni za mazoezi ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuhamasisha mazoezi kwa wananchi.

Shoo amesema uwanja huo bado haujazinduliwa rasmi kwa sababu unaendelea kujengwa na bado haujapewa jina rasmi lakini kwa sasa unatambulika kama Fresho Complex ambapo michezo mbalimbali itafanyika humo.

Meneja wa Uwanja wa Fresho Complex, Ombeni Kweka
ambaye ndiye aliyebuni ramani ya uwanja huo amesema umekamilika kwa asilimia 25 na unatarajiwa kukamilika kwa asilimia 100 kati ya mwaka 2022 na 2023 ukijumuisha bustani ya matunda, barabara ya kiwango cha lami, hoteli ya nyota tano, ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 1,000, eneo la kuogelea (Swimming pool) kwa ajili ya watoto na watu wazima.

“Uwanja wetu ni bora na wa kisasa,una mandhari nzuri, hakuna wa mfano kwa Kanda ya Ziwa, katika eneo la kuchezea (pitch) kuna mfumo wa mabomba yanayomwagilia maji kutoka chini na mfano hii tunaiona Ulaya, lakini pia Ujenzi wa majukwaa ukikamilika utakuwa na uwezo wa kubeba watazamaji 18,000 waliokaa na wengine kama 2,000 watakaosimama.

“Tumeanza kuujenga mwaka 2017 upana wake kwa eneo la kuchezea ni 68 kwa 110, sehemu zingine ambazo hazijakamilika ni eneo la kukimbilia (run away), bwawa la samaki, gym na vyumba vya kubadilishia nguo,” amesema.

Katika Bonanza la Maveterani wa timu ya Ammo Veterani/Jeshi Veterani, Mwanza Starehe Veterani,Unyanyembe Veterani na Shinyanga Veterani zilishuhudiwa mechi 12 ambapo kila timu ilicheza michezo mitatu.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo akichezea timu yake ya Shinyanga Veterani akiwa amevaa jezi namba 8 ameonesha makali yake baada ya kupachika bao moja katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mwanza Veterani.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali Justas Kitta akifungua Bonanza la Michezo lilokutanisha pamoja Maveterani kutoka Mikoa ya Mwanza (Mwanza Starehe), Tabora (Unyanyembe Veterani) na Shinyanga (Ammo Veterani /Jeshi Veterani na Shinyanga Veterani) katika Uwanja Mpya wa Kisasa uliopewa jina la ‘Fresho Complex’ unaojengwa na Kampuni ya Fresho Investment Company Ltd katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Juni 6,2020 . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanda ya Shinyanga, Kanali Justas Kitta akiipongeza Kampuni ya Fresho Investment Company Ltd kujenga Uwanja wa Michezo katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo akielezea lengo la kufanya Bonanza hilo la michezo kwa kukutanisha Timu za Maveterani ambapo amesema ni kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kutaka Watanzania wawe na afya nzuri na kuweza kupiga vita ugonjwa wa Corona ambapo watu wanaofanya mazoezi wana uwezakano mkubwa wa kushambuliwa na Virusi vya Corona.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo akielezea lengo la kujenga uwanja wa michezo wa ‘Fresho Complex’ ambapo alisema ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli katika kufanya watu wakiwemo ,wafanyakazi wa viwandani na serikalini wawe na afya nzuri kwa kufanya mazoezi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo akiwakaribisha wakazi wa Shinyanga na maeneo mengine kuutumia uwanjwa wa Fresho Complex . Amesema "Pamoja na kwamba uwanja huo utakuwa wa kibiashara lakini siku za Jumamosi atatoa bure kwa siku ambazo serikali imesema ni za mazoezi ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuhamasisha mazoezi kwa wananchi".
Meneja wa Uwanja wa Fresho Complex, Ombeni Kweka akielezea kuhusu Uwanja wa Fresho Complex. Amesema ujenzi wa uwanja huo wa kisasa,wenye mandhari nzuri,unatarajiwa kukamilika mwaka 2023 ukiwa una uwezo wa kubeba watazamaji zaidi ya 20,000.
Muonekano wa uwanja wa Fresho Complex wakati wa Bonanza la michezo lililokutanisha Maveterani kutoka Kanda ya Ziwa (Tabora, Shinyanga na Mwanza).
Muonekano wa uwanja wa Fresho Complex wakati wa Bonanza la michezo lililokutanisha Maveterani kutoka Kanda ya Ziwa (Tabora, Shinyanga na Mwanza).
Mechi ya Kwanza : Mchezo kati ya Unyanyembe Veterani kutoka Tabora na Jeshi Veterani (wenye jezi nyeupe) ukiendelea ambapo walitoka kwa kufungana bao 3-3.
Mchezo kati ya Unyanyembe Veterani kutoka Tabora na Jeshi Veterani (wenye jezi nyeupe) ukiendelea
Mchezo kati ya Unyanyembe Veterani kutoka Tabora na Jeshi Veterani (wenye jezi nyeupe) ukiendelea.
Dawati la ufundi timu ya Jeshi Veterani

Wachezaji timu ya Mwanza Starehe Veterani (wenye jezi za njano na kijani) na wachezaji wa Shinyanga Veterani wakijiandaa kuanza mechi ya awamu ya kwanza.
Wachezaji timu ya Mwanza Starehe Veterani (wenye jezi za njano na kijani) na wachezaji wa Shinyanga Veterani wakisalimiana kabla ya mechi ya kwanza kuanza.
Wachezaji timu ya Mwanza Starehe Veterani  wakiwa katika picha ya pamoja.
Wachezaji wa Shinyanga Veterani wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia waliosimama ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo.
Mchezo kati ya Mwanza Starehe Veterani (wenye jezi za njano na kijani) na Shinyanga Veterani ukiendelea katika Uwanja wa Fresho Complex ambapo Shinyanga Veterani iliibuka mshindi kwa kuichapa Mwanza Starehe Veterani magoli 3-2.
Kulia ni Mchezaji wa Timu ya Shinyanga Veterani, Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd, Fredy Shoo akiwa amevaa jezi namba 8. Katika mchezo huo alifanikiwa kupachika bao 1 na kuifanya Shinyanga Veterani ipate ushindi wa magoli 3-2.
Mchezo kati ya Mwanza Starehe Veterani (wenye jezi za njano na kijani) na Shinyanga Veterani ukiendelea katika Uwanja wa Fresho Complex ambapo Shinyanga Veterani iliibuka mshindi kwa kuichapa Mwanza Starehe Veterani magoli 3-2.
Mchezo kati ya Mwanza Starehe Veterani (wenye jezi za njano na kijani) na Shinyanga Veterani ukiendelea katika Uwanja wa Fresho Complex ambapo Shinyanga Veterani iliibuka mshindi kwa kuichapa Mwanza Starehe Veterani magoli 3-2.
Hatari katika lango Shinyanga Veterani...Mchezaji wa Mwanza Starehe Veterani akiipatia goli timu yake kwa njia ya penalti.
Dawati la ufundi Timu ya Shinyanga Veterani
Dawati la ufundi Timu ya Mwanza Starehe Veterani.
Mashabiki wakiwa uwanjani wakifuatilia mechi.
Waandishi wa habari na Afisa kutoka Kampuni ya Fresho wakifuatilia mechi uwanjani
Mashabiki wakiwa uwanjani.
Mashabiki wakishuhudiwa kabumbu uwanjani
Mashabiki wakishuhudiwa kabumbu uwanjani
Mashabiki wakishuhudiwa kabumbu uwanjani
Mashabiki wakishuhudiwa kabumbu uwanjani
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post