Mbunge wa Nkasi CCM, Ally Kessy ameliomba Bunge kumuongezea muda wa kutawala Rais John Magufuli hata kama yeye Rais hataki kwa kubadili Ibara inayoweka kikomo cha kipindi cha urais.
Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Kessy kuileta hoja hiyo baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika Bunge la 12 ambapo ameahidi kulishughulikia.
“Mheshimiwa Keissy ngoja tuende uchaguzi mkuu, turudi, na mimi naamini sote tunarudi. Hilo ulishikie uwe nalo moyoni, tutarudi hapa [bungeni] salama, azimio hilo utakuja kulileta wewe Mzee Keissy na litapita kwa kishindo, atake asitake [Rais Magufuli] tutaongeza muda,” Amesema Spika Job Ndugai
Itakumbukwa kuwa Rais Magufuli amekwisha kataa hadharani wazo la kuongeza muda wa kuongoza nchi.
Social Plugin