Wizara ya Madini leo imemtambua rasmi mchimbaji mdogo Saniniu Laizer kuwa Bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili ya Tanzanite yenye thamani ya Tsh. Billion 7.8.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kuwa mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.
“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo” amesema Prof. Msanjila
Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.
Social Plugin