Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2020.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma Juni 8,2020 na , kaimu mkurugenzi wa sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bi Ruth Minja wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Amesema kuwa mfumuko wa Taifa umeshukua kufuatia kushuka kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Mei 2020.
Akizungumzia hali ya Mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa nchini Kenya mfumuko wa bei ulioishia mwezi Mei umepungua hadi kufikia asilimia 5.47 kutoka asilimia 5.62 kwa mwezi ulioishia April 2020 huku Nchini Uganda, mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Mei mwaka huu, umepungua hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi April 2020.
Ikumbukwe kuwa Ofisi ya taifa ya takwimu (nbs) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 iliyopewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa wa taarifa za kitakwimu nchini.
Social Plugin