Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amezindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children leo Ijumaa Juni 12,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
****
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amezindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children wenye lengo la kuboresha ushiriki wa wananchi na asasi za Kiraia katika mijadala jumuishi ya masuala ya uchumi na usimamizi wa rasilimali fedha.
Mkutano huo wa kutambulisha mradi mpya umefanyika leo Ijumaa Juni 12,2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa na Manispaa ya Shinyanga.
Alisema Mradi huo umejikita katika kutoa elimu ya ushiriki wa wananchi na wadau katika michakato ya uandaaji wa Mipango na Bajeti kwa kila Halmashauri ambapo ushiriki huo utatoa fursa kwa wananchi kutoa maoni na mapendekezo ya vipaumbele katika masuala mbalimbali ikiwemo mambo yanayolenga ustawi wa watoto.
“Katika uandaaji wa bajeti za kila mwaka za halmashauri,mchakato huanzia katika ngazi za vijiji ambako ndiko kwenye mahitaji hasa ya vipaumbele. Bado kuna changamoto ya ushiriki mdogo wa wananchi wakati wa maandalizi ya bajeti zetu. Naamini mradi huu utasaidia kuongeza ushiriki huo wa wananchi naa wadau wengine ili kuwa na bajeti yenye uhalisia”,alisema Telack.
“Kwa kuwa mradi utahusisha kufanya tathmini mbalimbali na uchambuzi wa bajeti kwa kuangalia utekelezaji wake hasa kwa kuzingatia masuala muhimu yanayohusu maisha ya watoto.Namuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kutoa ushirikiano wa kutosha kuanzia ngazi ya halmashauri mpaka kitongoji ili mradi uwe na mafanikio yaliyotarajiwa”,alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo wa mkoa aliliomba shirikala Save The Children kuongeza wigo wa mradi huo badala ya Manispaa ya Shinyanga pekee huku akiwataka wadau na viongozi wa mkoa na Manispaa kutoa ushirikiano wa kutosha wakati wa utekelezaji wa mradi huo ili kuimarisha ustawi wa watoto.
“Ni jukumu la kila mmoja wetu kumlinda mtoto tangu akiwa tumboni hadi anazaliwa. Msitoe elimu kwa kupotosha watoto. Tulee watoto wetu katika misingi ya Utanzania na siyo vinginevyo. Watoto wanapoanza shule tuhakikishe hakuna mtoto anakatisha masomo yake. Tuwalinde na kuwasaidia watoto wetu”,aliongeza.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children Alex Enock alisema mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya tayari umeanza kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba 2021.
“Mbali na mradi huu kutekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga pia unatekelezwa Unguja – Zanzibar, na Mbozi – Songwe ambapo walengwa ni halmashauri za wilaya,watoto,waandishi wa habari na asasi za kiraia”,alieleza Enock.
“Mradi huu una sura mpya katika kufanya kazi na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuboresha mipango na kutoa elimu kwa jamii kutambua jukumu lao katika kutoa ushawishi na uelewa juu ya mipango na bajeti ya serikali ili wananchi waelewe serikali inakwenda kutekeleza nini katika mwaka wa fedha”,alisema.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Kuzindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children leo Ijumaa Juni 12,2020 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Albert Msovela. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwasisitiza wadau na wananchi kulinda na kutunza watoto kwani ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha watoto wanakuwa salama muda wote.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza wakati wa Kuzindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.
Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale na Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children , Alex Enock wakiwa ukumbini wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack Kuzindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akiwataka wadau wa haki za watoto kutojihusisha na masuala la kisiasa wanapotekeleza majukumu yao ya kusaidia jamii.
Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children , Alex Enock akielezea lengo la mradi huo ambao una lengo la kuboresha ushiriki wa wananchi na asasi za Kiraia katika mijadala jumuishi ya masuala ya uchumi na usimamizi wa rasilimali fedha.
Mratibu wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children , Alex Enock akiishukuru serikali kwa ushirikiano inaoendelea kulipatia shirika la Save The Children katika kutekeleza miradi ya maendeleo mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Albert Msovela akizungumza wakati wa Mkutano wa Kutambulisha/ Kuzindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza wakati wa Mkutano wa Kutambulisha/ Kuzindua rasmi Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.

Wadau na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.

Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.
Wadau na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.
Wadau na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Mijadala Jumuishi katika Masuala ya Uchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha unaotekelezwa na Shirika la Save The Children.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin