Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSANII WAKAZI AJITOSA KWENYE UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO

Msanii wa HipHop Bongo Wakazi ametia nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ukonga kupitia chama cha ACT- Wazalendo  kwenye uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu. 




Wakazi ameeleza nia hiyo leo Juni 20, 2020 kwenye mkutano wa chama hicho unaofanyika jijini Dar es salaam.

Wakazi amesema amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu wa masuala ya haki na usawa hivyo ameona ni wakati sasa wa kuwa kiongozi.

”Kwasababu nimepata heshima ya kuitwa hapa mbele ya mkutano naomba nitumie nafasi hii kutangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika Jimbo langu la Segerea”, amesema.

Hivi karibuni Wakazi alikabidhiwa kadi ya chama hicho na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com