Aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Redio cha Clouds FM Hamis Mandi maarufu B Dozen amejiunga na Kituo cha redio cha EFM- Tanzania.
Mandi ambaye anafahamika zaidi kwa jina la utangazaji la B-Dozen (The Navigator, Msafiri) kwa muda mrefu alikuwa akiongoza kipindi cha XXL cha Clouds FM, pamoja na vingine.
Kupitia ukurasa wao wa Instagram, E-FM wameandika mbobezi huyo wa utangazaji amejiunga nao, na kwamba kinachofuata ni kupaa juu, na kuhakikisha mafanikio zaidi kwa Tanzania.
Social Plugin