Chama cha NCCR-Mageuzi kimetangaza ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu katika chama hicho kuanzia leo hadi Julai 8 mwaka huu.
Akitangaza ratiba hio, Katibu Mkuu wa chama hicho, Elizabeth Mhagama amesema kuwa fomu ya kugombea urais itatolewa katika Makao Makuu ya chama hicho huku fomu za ubunge na udiwani zikitolewa katika kata na majimbo husika.
“Kwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watachukua fomu hapa Makao Makuu itatolewa na Katibu Mkuu, kwa wagombea urais Zanzibar watachukua fomu hizo katika halmashauri kuu maalum iliyopo Zanzibar huko yupo Naibu Katibu Mkuu Zanzibar vile vile kwa wawakilishi” amesema Mhagama
NCCR-Mageuzi imetangaza ratiba hiyo wakati ambapo vyama mbalimbali vimeshatangaza ratiba zao za kuchukua na kurejesha fomu ,sambamba na kutangaza nia kuwania nafasi mbalimbali.
Social Plugin