Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako ametoa muda wa hadi kufika Ijumaa wiki hii ambayo itakuwa Juni 5, 2020, vyuo vyote vya elimu ya juu hapa nchini viwe vimemaliza kuwapa fedha za kujikimu wanafunzi wote na si vinginevyo.
Amesema hayo leo Juni 6, 2020 wakati akizungumza baada ya kukabidhi magari manne kwa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT).
Ndalichako amesema, serikali haitakuwa na mswalia mtume katika hili kwa kuwa tayari ilishatoa fedha hizo na hakuna sababu ya kuchelewa kuwapa wanafunzi fedha hizo
"Hakuna sababu ya kuwacheleweshea fedha wanafunzi wakati serikali imeshatoa Sh.bil 122.Rais alishatoa maelekezo na lazima yatekelezwe.Sasa ole wao vyuo vitakavyokuwa havijatekeleza agizo .Suala la wanafunzi kukataa kusaini siyo kweli, hatutakuwa na msalia mtume.
"Ifikapo Ijumaa wiki hii wanafunzi wote wa vyuo vikuu wawe wameshapata fedha zao za kujikimu, hatutakuwa na msamaha kwa vyuo ambavyo vitakuwa havijatekeleza agizo hilo.
"Kama kutakuwa na wanafunzi ambao watakuwa hawajasaini fedha za kujikimu achaneni nao, wapeni ambao wameshaini"-Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako
Vyuo vimefunguliwa Juni 1, 2020 baada ya kusimama kutokana na janga la Corona. Serikali tayari imeshathibitisha kuingiza fedha za mikopo kwa wanafunzi hivyo kuacha jukumu kwa vyuo kukamilisha kuwapatia wanafunzi.
Social Plugin