Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga (2015-2020) ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Madiwani CHADEMA Kanda ya Serengeti mkoa wa Simiyu Mara na Shinyanga, Emmanuel Ntobi ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ntobi ametangaza leo Jumamosi Juni 27,2020 kuanza mbio za kuusaka ubunge kupitia CHADEMA akieleza kuwa atashukuru endapo Chama chake kitampa ridhaa ya kuwa mgombea Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Social Plugin